Sikika Wins National Board of Accountants and Auditors Award
The National Board of Accountants and Auditors (NBAA), Tanzania adopted international accounting and auditing standards in 2004. However, many organizations are facing the challenge of compliance with these standards in preparing financial reports. To recognize organizations which achieve these high standards, the NBAA has established a national competition for organizations to compete for the award of the best-presented financial statements.
Mafunzo ya SAM yachangia Mabadiliko Zahanati Kilolo
Zahanati ya Kilolo, iliyopo wilayani Kilolo, ilikuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali za miundombinu ikiwemo kutokuwa na umeme, kichomea taka, shimo la kutupia kondo la uzazi na kukosa jengo la upasuaji. Changamoto hizo na zingine kwa sasa zimepatiwa ufumbuzi na Halmashauri.
Mafunzo ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM), yaliyotolewa na Sikika mwaka 2016, yamechangia kuiwezesha timu ya SAM kushirikiana na uongozi wa wilaya ya Kilolo kuleta mabadiliko. Matokeo mengine chanya yaliyopatikana kutokana na ufuatiliaji wa timu ya SAM kwa kushirikiana na Halmashauri ya Kilolo, ni ujenzi wa jengo la upasuaji ambalo pia limekamilika.
Umakini kujaza fomu wachangia ongezeko la dawa
Ujazaji sahihi wa fomu za taarifa za matumizi na maombi ya dawa maarufu kama Report and Requisition (R&R) katika kituo cha afya Mirerani, wilayani Simanjiro umechangia kuondoa changamoto ya upungufu wa dawa uliotokana na makosa wakati wa kuzijaza.
Wilaya ya Simanjiro imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa muda mrefu, hivyo kuathiri upatikaji wa huduma bora za afya kwa wananchi. Ufuatiliaji uliofanywa na Sikika mwaka 2016, uligundua kwamba, upungufu wa dawa, pamoja na sababu zingine, ulichangiwa pia na ujazaji usio sahihi wa fomu za R&R, hivyo kusababisha ucheleweshaji wa kupokea dawa vituoni. Ufuatiliaji huu ulilenga kubaini changamoto zinazochangia tatizo la upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma..
Expectant mother in Kondoa escapes death!
To date, Asia Aboubakar is still fighting back tears when she narrates about how her life and that of her son was saved by Kondoa SAM (Social Accountability Monitoring) team members.
Asia, a young mother from Kwamtoro Ward in Kondoa district, decided to name her beautiful and healthy child SAM, as a way of showing her gratitude to the team that saved their lives. “ If it wasn’t for the human decision and sacrifice made by SAM team, my son and I would be dead by now”.