Matumizi yasiyo ya lazima kuongezeka kufika Tsh. 537bn kwa mwaka wa fedha 2010/11

Pamoja na ufinyu wa bajeti ya taifa, kuna baadhi ya vipengele katika bajeti hii ambavyo
vinaonekana kuwa havina tija kutokana kwamba haviwanufaishi watanzania walio wengi.
Ni bahati kwamba serikali pia inalitambua tatizo hili la matumizi yasiyo ya lazima kwa wananchi
walio wengi na kupitia viongozi wa juu wa Serikali kama Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda,
ilidhamiria kuongeza udhibiti wa matumizi hayo.
Jumla ya matumizi yote yasiyo ya lazima katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali yalipungua
kutoka shilingi za kitanzania bilioni 684 katika mwaka wa fedha wa 2008/09 hadi shilingi za
kitanzania bilioni 530 katika mwaka wa fedha 2009/10, ambapo ni punguzo la asilimia 22.4.
Lakini, kwa mwaka wa fedha 2010/11. Matumizi haya yasiyo ya lazima yanategemea
kuongezeka kidogo na kufikia kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 537, hatua ambayo
inapingana na dhamira ya serikali ya kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima.

Download file .pdf

Leave a Reply

Choose your Style
Layout Style
Predefined Colors * You can use Unlimited Colors