Send SMS: 0688493882

Follow us:

Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu nchini (LHRC), Bi. Helen Kijo Bisimba (Kushoto) na Balozi wa Sweden  nchini Tanzania Bi. Katarina Rangitt wakikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Haki za Binadamu  kwa mwaka 2017. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa na ongezeko kubwa la ukiukwaji wa haki nchini. Haki 5 zilizovunjwa  zaidi mwaka 2017 ni Haki ya Kuishi, Haki dhidi ya Ukatili, Haki ya na Usalama wa Mtu, Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa  kukusanyika na Uhuru wa Kujumuika. #HumanRightsReport

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya akitoa muongozo    wa namna ya uwasilishwaji wa mada mbalimbali katika mkutano wa  Wataalam kuhusu Mapitio ya Sekta ya Afya kwa  mwaka 2017 - Technical Review Meeting (TRM). 

Mkuu wa Ofisi ya Kanda Sikika - Dodoma, Bw. Richard Msittu akitoa utambulisho wa Shirika  kwa Wadau wa Afya      katika Mkutano - Manispaa ya Kigoma Ujiji.