Acheni matumizi ya lugha chafu: Watumishi na wafanyakazi wa Afya, July 2010

Wataalam wa Afya wameonywa kuacha kutumia lugha chafu wanapohudumia wagonjwa kwani kwa
kufanya hivyo kunaathiri tabia ya kutafuta matibabu na kuwakatisha tamaa wagonjwa wanaokwenda
kupata huduma katika vituo vya huduma za afya vya umma.

Hivi karibuni, Mamlaka ya Mji wa Morogoro ilifanyia kazi malalamiko ya wananchi juu ya watumishi na
wafanyakazi wa afya katika vituo mbalimbali vya huduma mkoani humo ambao wamekuwa wakitoa
huduma chini ya kiwango na kutoa lugha chafu kwa wagonjwa.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mh. Issa
Machibya amewaambia wauguzi na waganga katika mkutano kwamba amepokea malalamiko mengi
ofisini kwake kuhusu utoaji huduma za afya na unyanyasaji wa wagonjwa.

Lugha chafu kwa wauguzi huthibitisha mmomonyoko wa maadili ya kazi na ukosefu wa wito wa kazi
hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa kutoa huduma kwa wagonjwa kwa upendo na
unyenyekevu kama ilivyobainishwa katika sera za serikali na Mkataba wa huduma kwa mteja. Sikika
inapenda kuwakumbusha watoa huduma hawa kuwa, mawasiliano ni muhimu hasa katika taaluma ya
afya kutokana na matokeo yake. Kutokuwepo na mfumo thabiti wa mawasiliano baina ya watoa na
watumia huduma kunachangia kwa kiasi kikubwa kupotea kwa muda, kutoelewana, mahusiano mabaya
na kukwamisha uboreshaji wa huduma. Katika huduma za afya, mawasiliano ni muhimu zaidi sababu
lengo kuu ni kujali wananchi, wagonjwa na afya zao na wala si namba, majengo ama mauzo ya huduma
hizo. Hivyo basi, mawasiliano mazuri, duni ama kutokuwepo kabisa mawasiliano kuna athari kubwa kwa
watumia huduma.

Download file .pdf

Leave a Reply

Choose your Style
Layout Style
Predefined Colors * You can use Unlimited Colors